Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 37

Saba 34:37

سبإ

وَمَآ أَمْوَٰلُكُمْ وَلَآ أَوْلَـٰدُكُم بِٱلَّتِى تُقَرِّبُكُمْ عِندَنَا زُلْفَىٰٓ إِلَّا مَنْ ءَامَنَ وَعَمِلَ صَـٰلِحًا فَأُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ جَزَآءُ ٱلضِّعْفِ بِمَا عَمِلُوا۟ وَهُمْ فِى ٱلْغُرُفَـٰتِ ءَامِنُونَ

Maana

Na si mali zenu wala watoto wenu watakaowasongesha karibu na sisi, muwe karibu sana, isipokuwa yule aliyeamini na akatenda mema. Hao basi watapata malipo maradufu kwa yale waliyoyafanya. Nao watakuwa salama katika maghorofa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na si mali yenu wala watoto wenu watakao kukaribisheni kwetu muwe karibu, isipo kuwa aliye amini na akatenda mema. Hao basi watapata malipo mardufu kwa walio yafanya. Nao watakuwa salama katika maghorofa. [37]

[37] Wala mali yenu wala watoto wenu sio jambo la kukurubisheni kwetu mkawa karibu. Lakini ambaye Imani yake imethibiti, na akawa anatenda mema, basi watu kama hao ndio watapata thawabu mara mbili kwa waliyo yatenda. Na Peponi watakuwa ni watu wa juu na wenye amani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hayakuwa mali yenu na watoto wenu ni vitu vya kuwafanya nyinyi muwe karibu na sisi, na daraja zenu ziwekwe juu, lakini wenye kumuamini Allah Mtukufu na wakafanya matendo mema, basi hao watapata malipo ya nyongeza: kwa jema moja kwa kumi mfano wake mpaka kiwango cha nyongeza Anachokitaka Allah Mtukufu. Na wao watakuwa kwenye Pepo ya juu, wakiwa wamesalimika na adhabu, kifo na mambo ya huzuni.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net