Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 36

Saba 34:36

سبإ

قُلْ إِنَّ رَبِّى يَبْسُطُ ٱلرِّزْقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقْدِرُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

Maana

Sema, "Hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki amtakaye na humdhikisha amtakaye. Lakini watu wengi hawajui."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki na humdhikisha amtakaye. Lakini watu wengi hawajui. [36]

[36] Ewe Nabii! Waambie: Hakika aliye niumba humkunjulia riziki amtakaye, katika wanao muasi na wanao mt'ii. Na humdhikisha amtakaye. Wala hiyo si dalili ya kuwa Yeye yuradhi na mtu au anamchukia. Lakini watu wengi hawajui haya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema uwaambie, ewe Mtume, «Hakika Mola wangu Anawakunjulia riziki hapa duniani anaowataka miongoni mwa waja Wake, na anawapunguzia Anaowataka, si kwa mapenzi wala chuki, lakini Anafanya hivyo kwa kuwatahini. Lakini wengi wa watu hawajui kwamba huo ni mtihani kwa waja Wake kwa kuwa wao hawazingatii».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net