Saba 34:35
سبإوَقَالُوا۟ نَحْنُ أَكْثَرُ أَمْوَٰلًا وَأَوْلَـٰدًا وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ
Na wakasema, "Sisi tuna mali nyingi zaidi na watoto, wala sisi hatutaadhibiwa."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wakasema: Sisi tuna mali mengi zaidi na watoto, wala sisi hatutaadhibiwa. [35]
[35] Na husema kwa kujipa: Sisi tuna mali mengi zaidi na watoto. Wala hatutaadhibiwa Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanasema, «Sisi ni wengi zaidi wa mali na watoto, na Allah Mtukufu hakutupa neema hizi isipokuwa ni kuwa anaridhika na sisi, na sisi si wenye kuadhibiwa duniani wala Akhera».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net