Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 62

Al-Ahzaab 33:62

الأحزاب

سُنَّةَ ٱللَّهِ فِى ٱلَّذِينَ خَلَوْا۟ مِن قَبْلُ ۖ وَلَن تَجِدَ لِسُنَّةِ ٱللَّهِ تَبْدِيلًا

Maana

Hii ni ada ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa kwa wale waliopita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika ada ya Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hii ni ada ya Mwenyezi Mungu iliyo kuwa kwa wale walio pita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika ada ya Mwenyezi Mungu. [62]

[62] Mwendo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu tangu zamani, kwa walio kuwa wakiwafanyia unaafiki Manabii na Mitume, na wakiasi, ni kuwa huuwawa kila wanapo kutikana. Wala mwendo wa Mwenyezi Mungu haugeuki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Huu ndio mpango wa Allah Mtukufu na njia Yake kuhusu ummah waliopita, ni kuwa watekwe na wawe ni wenye kuuawa popote walipo. Na hutapata, ewe Nabii, mageuzi wala mabadiliko katika njia ya Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net