Al-Ahzaab 33:63
الأحزابيَسْـَٔلُكَ ٱلنَّاسُ عَنِ ٱلسَّاعَةِ ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ ٱللَّهِ ۚ وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ ٱلسَّاعَةَ تَكُونُ قَرِيبًا
Watu wanakuuliza habari ya Saa ya Kiyama. Sema: "Hakika elimu yake iko kwa Mwenyezi Mungu." Na nini kitakujulisha, pengine hiyo Saa iko karibu?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Watu wanakuuliza khabari ya Saa (ya Kiyama). Sema: Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu. Na nini kitakujuvya? Pengine hiyo Saa iko karibu. [63]
[63] Watu wanakuuliza lini itasimama Saa ya Kiyama. Waambie hao: Hakika ujuzi wa wakati wake uko kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Na nini kitakujuvya? Pengine wakati wa kusimama Saa ya kiyama upo karibu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanakuuliza watu, ewe Mtume, kuhusu kipindi cha Kiyama kwa njia ya kukiona ni kitu ambacho ni mbali kutokea na kwa njia ya kukikanusha. Waambie, «Hakika ya mambo ni kwamba Ujuzi wa kipindi cha Kiyama uko kwa Allah Mtukufu.» Na ni lipi linalokujuza wewe, ewe Mtume kwamba huenda Kiyama kikawa karibu?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net