Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 52

Al-Ahzaab 33:52

الأحزاب

لَّا يَحِلُّ لَكَ ٱلنِّسَآءُ مِنۢ بَعْدُ وَلَآ أَن تَبَدَّلَ بِهِنَّ مِنْ أَزْوَٰجٍ وَلَوْ أَعْجَبَكَ حُسْنُهُنَّ إِلَّا مَا مَلَكَتْ يَمِينُكَ ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ رَّقِيبًا

Maana

Baada ya hawa hawakuhalalikii wewe wanawake wengine, wala kuwabadilisha kwa wake wengine, ingawa uzuri wao ukikupendeza, isipokuwa yule uliyemmiliki kwa mkono wako wa kulia. Na Mwenyezi Mungu anachunga kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Baada ya hawa hawakuhalalikii wewe wanawake wengine, wala kuwabadilisha kwa wake wengine ingawa uzuri wao ukikupendeza; isipo kuwa yule uliye mmiliki kwa mkono wako wa kulia. Na Mwenyezi Mungu anachungua kila kitu. [52]

[52] Hawakuhalalikii wanawake wengine baada ya hawa, wala kuwapa t'alaka kwa ajili ya kuwabadilisha kwa wengine uwatakao, hata wakikupendeza kwa uzuri wao. Lakini Mwenyezi Mungu amekuhalalishia wajakazi ulio wamiliki kwa mkono wako. Na Mwenyezi Mungu anachungua kila kitu, na anakihifadhi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Haifai kwako kuwaoa wanawake baada ya wake zako walio mama wa Waumini, na usiwaache wao ukawaoa wengine badala yao, kwa kuwakirimu na kushukuru mazuri waliyoyatenda ya kumchagua Allah Mtukufu na Mtume Wake na Nyumba ya Akhera, hata kama utavutiwa na uzuri wa hao wanawake wengine, isipokuwa kile ambacho mkono wako wa kulia umemiliki, miongoni mwa wajakazi, kwani hao ni halali kwako. Na Allah Mtukufu anakiona kila kitu, hakuna chochote kilicho nje ya ujuzi Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net