Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 51

Al-Ahzaab 33:51

الأحزاب

تُرْجِى مَن تَشَآءُ مِنْهُنَّ وَتُـْٔوِىٓ إِلَيْكَ مَن تَشَآءُ ۖ وَمَنِ ٱبْتَغَيْتَ مِمَّنْ عَزَلْتَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكَ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰٓ أَن تَقَرَّ أَعْيُنُهُنَّ وَلَا يَحْزَنَّ وَيَرْضَيْنَ بِمَآ ءَاتَيْتَهُنَّ كُلُّهُنَّ ۚ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ مَا فِى قُلُوبِكُمْ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَلِيمًا

Maana

Unaweza kuakhirisha zamu kwa umtakaye katika wao, na umsongeze karibu umtakaye. Na kama ukimtaka yule uliyemtenga, basi si vibaya kwako. Kufanya hivi kutapelekea yaburudike macho yao, wala wasihuzunike, na wawe radhi juu ya kile unachowapa wao wote. Na Mwenyezi Mungu anajua yaliyomo nyoyoni mwenu, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Unaweza kuakhirisha zamu kwa umtakaye katika wao, na umsogeze umtakaye. Na kama ukimtaka yule uliye mtenga, basi si vibaya kwako. Kufanya hivi kutapelekea yaburudike macho yao, wala wasihuzunike, na wawe radhi juu ya kile unacho wapa wao wote. Na Mwenyezi Mungu anajua yaliyomo nyoyoni mwenu, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima. [51]

[51] Unaweza kumuakhirisha umtakaye katika kugawa zamu, na ukamjongeza umtakaye. Na kumtaka uliye muakhirisha zamu yake hapana lawama juu yako. Hivyo kuachiliwa utakavyo wewe yakaribia zaidi kupelekea furaha yao na baada ya kuwahuzunikia, na wao wote wawe radhi kwa ulio wapa. Na Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo ndani ya nyoyo zenu, ya kuudhika au kuridhika kwa aliyo kufanyieni sharia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua yaliomo vifuani, Mpole hafanyi papara kuadhibu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Unamkalisha nyuma unayemtaka miongoni mwa wake zako katika ugawaji wa kulala, na unamleta karibu nawe unayemtaka miongoni mwao. Na yoyote unayemtaka kati ya wale uliochelewesha ugawaji wao, huna dhambi katika hilo. Kwani hiyari hiyo iko karibu zaidi ya kuwafanya wao wafurahike wala wasihuzunike na waridhike wote kwa kile ulichowagawia. Na Allah Mtukufu Anavijua vilivyomo ndani ya nyoyo za wanaume, vya kuelemea upande wa baadhi ya wake na kutoelekea upande wa wengine. Na Allah Mtukufu ni mjuzi wa yaliyomo ndani ya nyoyo, ni Mpole, Hafanyi haraka ya kuwatesa wanaomuasi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net