Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 49

Al-Ahzaab 33:49

الأحزاب

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا نَكَحْتُمُ ٱلْمُؤْمِنَـٰتِ ثُمَّ طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ فَمَا لَكُمْ عَلَيْهِنَّ مِنْ عِدَّةٍ تَعْتَدُّونَهَا ۖ فَمَتِّعُوهُنَّ وَسَرِّحُوهُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا

Maana

Enyi mlioamini, mkiwaoa wanawake, Waumini, kisha mkawapa talaka kabla ya kuwagusa, basi hamna eda juu yao mtakayohesabu. Basi wapeni cha kuwaliwaza, na muwaache kwa wema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

nyi mlio amini! Mkiwaoa wanawake, Waumini, kisha mkawapa t'alaka kabla ya kuwagusa, basi hamna eda juu yao mtakayo ihisabu. Basi wapeni cha kuwaliwaza, na muwawache kwa kuwachana kwa wema. [49]

[49] Enyi mlio amini! Mkifunga ndoa na wanawake Waumini, kisha mkawat'aliki kabla ya hamjawaingilia, basi haiwalazimu eda wao mkawa mnaihisabu. Basi wapeni kitu katika mali kwa kuwapoza. Na mwatoe majumbani kwenu bila ya kuwaletea madhara yoyote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata sheria zake kivitendo, mfungapo ndoa na wanawake na msiwaingilie, kisha mkawaacha kabla hamjawaingilia, basi hawalazimiki wawakalie eda ya nyinyi kuwahesabia, basi wapeni kitu cha kuwastarehesha katika mali yenu kulingana na uwezo mlionao ili kuwapa maliwazo, na waachieni washike njia waende zao pamoja na sitara nzuri, bila ya udhia wala madhara.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net