Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 48

Al-Ahzaab 33:48

الأحزاب

وَلَا تُطِعِ ٱلْكَـٰفِرِينَ وَٱلْمُنَـٰفِقِينَ وَدَعْ أَذَىٰهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلًا

Maana

Wala usiwatii makafiri na wanafiki, na usijali udhia wao. Nawe mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mtegemewa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala usiwat'ii makafiri na wanaafiki, na usijali udhia wao. Nawe mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mtegemewa. [48]

[48] Na wala usiwafuate makafiri na wanaafiki, wala usijishughulishe na maudhi yao. Na mfanye Mwenyezi Mungu ndiye Wakili wako wa kumtegemea kukulinda na madhara yao na shari zao. Na Mwenyezi Mungu anakutosha kabisa kuwa ndiye Mtegemewa wa kukukifia na kukukinaisha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na usilitii, ewe Nabii, neno la kafiri au mnafiki na uuache udhia wao, na hilo lisikuzuie kufikisha ujumbe, na kuwa na imani na Allah Mtukufu katika mambo yako yote, na umtegemee Yeye, kwani Yeye Atakutosheleza yanayokutia simanzi miongoni mwa mambo yote ya ulimwengu na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net