Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 46

Al-Ahzaab 33:46

الأحزاب

وَدَاعِيًا إِلَى ٱللَّهِ بِإِذْنِهِۦ وَسِرَاجًا مُّنِيرًا

Maana

Na mwitaji kumwendea Mwenyezi Mungu kwa idhini yake, na taa yenye kutoa nuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mwitaji kumwendea Mwenyezi Mungu kwa idhini yake, na taa yenye kutoa nuru. [46]

[46] Na umetumwa uwe ni mwenye kuwaita viumbe vyote vimwendee Mwenyezi Mungu kwa amri yake. Na uwe ni taa ya uwongofu kuwaongoa kwa nuru yake waliopo katika kiza cha shaka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na uwe ni mlinganizi kwenye kumpwekesha Allah Mtukufu na kumuabudu Yeye Peke Yake, na uwe ni taa yenye kung’ara kwa anayetaka kupata mwangaza kwako. Kwani jambo lako la haki ambalo umekuja nalo liko wazi kama vile jua katika kuchomoza na kutoa mwangaza, hakuna mwenye kulikanusha isipokuwa mshindani.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net