Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 45

Al-Ahzaab 33:45

الأحزاب

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ إِنَّآ أَرْسَلْنَـٰكَ شَـٰهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا

Maana

Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekutuma uwe shahidi na mbashiri na mwonyaji.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekutuma uwe shahidi na mbashiri na mwonyaji, [45]

[45] Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekutuma kwa watu wote uwapelekee ujumbe wa Uislamu. Ushuhudie Haki, na uwabashirie Waumini kwamba watapata kheri na thawabu, na uwaonye makafiri kuwa watapata mwisho muovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ewe Nabii! Sisi tumekutuma uwe ni shahidi juu ya ummah wako kwa kuwafikishia ujumbe, na kuwabashiria Waumini miongoni mwao rehema na Pepo, na uwe ni mwenye kuwaonya na Moto waasi na wakanushaji.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net