Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 44

Al-Ahzaab 33:44

الأحزاب

تَحِيَّتُهُمْ يَوْمَ يَلْقَوْنَهُۥ سَلَـٰمٌ ۚ وَأَعَدَّ لَهُمْ أَجْرًا كَرِيمًا

Maana

Maamkizi yao siku ya kukutana naye yatakuwa Salama! Na amewaandalia malipo ya ukarimu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Maamkiano yao siku ya kukutana naye yatakuwa: Salama! Na amewaandalia malipo ya ukarimu. [44]

[44] Maamkio yao siku watakapo kutana naye ni: Amani na Salama kwao. Na amewatengezea kwa vitendo vyao ujira wa ukarimu utakao waonyesha fadhila zake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Maamkizi ya hawa Waumini kutoka kwa Allah Mtukufu huko Peponi Siku ya wao kukutana na Yeye ni Salām na amani kwao kutokana na adhabu ya Allah Mtukufu. Na Amewaandalia wao malipo Mazuri, nayo ni Pepo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net