Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 43

Al-Ahzaab 33:43

الأحزاب

هُوَ ٱلَّذِى يُصَلِّى عَلَيْكُمْ وَمَلَـٰٓئِكَتُهُۥ لِيُخْرِجَكُم مِّنَ ٱلظُّلُمَـٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ ۚ وَكَانَ بِٱلْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا

Maana

Yeye ndiye anayekurehemuni na Malaika wake ili akutoeni gizani hadi kwenye nuru. Naye ni Mwenye kuwarehemu sana Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye na Malaika wake ndio wanakurehemuni ili kukutoeni gizani mwende kwenye nuru. Naye ni Mwenye kuwarehemu Waumini. [43]

[43] Na Yeye ndiye aliye kuahidini kukupeni rehema yake na upole wake. Na Malaika wake wanakuombeeni maghfira na uwongofu, ili Mwenyezi Mungu akutoeni kwenye giza la ukafiri na upotovu, mwendee kwenye nuru na ut'iifu. Na Mwenyezi Mungu hakika ni Mkuu wa kuwarehemu Waumini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yeye Ndiye Anayewarehemu na kuwasifu, na Malaika Wake wanawaombea dua, ili awatoe kutoka kwenye giza la ujinga na upotevu kuwaelekeza kwenye nuru ya Uislamu.Na ni Mwenye kuwarehemu Waumini duniani na Akhera, hawaadhibu wao maadamu wao wanaendelea kumtii na kumtakasa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net