Al-Ahzaab 33:42
الأحزابوَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا
Na mtakaseni asubuhi na jioni.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mtakaseni asubuhi na jioni. [42]
[42] Enyi ambao mmeamini! Msifuni Mwenyezi Mungu kwa namna mbali mbali za sifa, na mfanye hayo kwa wingi. Na mtakaseni na kila kisicho kuwa laiki naye mwanzo wa mchana na mwisho wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na zishughulisheni nyakati zenu kwa kumtaja Allah Mtukufu, Aliyetukuka, asubuhi na jioni, baada ya Swala za faradhi na nyakati za matukio maalumu na zenye sababu, kwani huko kumtaja Allah Mtukufu ni ibada iliowekwa na Sheria, inapelekea kwenye mapenzi ya Allah Mtukufu na kujizuia na madhambi, na inasaidia kila kheri.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net