Al-Ahzaab 33:38
الأحزابمَّا كَانَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ مِنْ حَرَجٍ فِيمَا فَرَضَ ٱللَّهُ لَهُۥ ۖ سُنَّةَ ٱللَّهِ فِى ٱلَّذِينَ خَلَوْا۟ مِن قَبْلُ ۚ وَكَانَ أَمْرُ ٱللَّهِ قَدَرًا مَّقْدُورًا
Hapana ubaya kwa Nabii kufanya aliyomhalalishia Mwenyezi Mungu. Huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa wale waliopita zamani. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni mipango iliyokwisha pangwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hapana ubaya kwa Nabii kufanya aliyo mhalalishia Mwenyezi Mungu. Huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa walio pita zamani. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni kudura iliyo kwisha kadiriwa. [38]
[38] Nabii hana makosa kutenda kitendo alicho muamrisha Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ameweka mwendo huo kwa Manabii walio tangulia, kuwa wasipige marfuku alicho wahalalishia na akawakunjulia. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni kupitisha alicho pitisha, na hukumu iliyo thibiti.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Haikuwa ni dhambi kwa Nabii Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), katika kile Alichomhalalishia Allah Mtukufu cha kumuoa mke wa mwanawe wa kujipachika baada ya kumuacha, kama vile alivyowahalalishia hilo Manabii kabla yake, ni mwenendo uliowekwa na Allah Mtukufu kwa wale waliopita kabla. Na kwa kweli, amri ya Allah Mtukufu ni mpango uliokadiriwa, hauna budi kutokea.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net