Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 39

Al-Ahzaab 33:39

الأحزاب

ٱلَّذِينَ يُبَلِّغُونَ رِسَـٰلَـٰتِ ٱللَّهِ وَيَخْشَوْنَهُۥ وَلَا يَخْشَوْنَ أَحَدًا إِلَّا ٱللَّهَ ۗ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ حَسِيبًا

Maana

Hao wa zamani, waliokuwa wakifikisha jumbe za Mwenyezi Mungu na wanamwogopa Yeye, na wala hawamwogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mhasibu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

(Hao wa zamani) walio kuwa wakifikisha risala za Mwenyezi Mungu na wanamwogopa Yeye, na wala hawamwogopi yeyote isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye atoshaye kuhisabu. [39]

[39] Manabii hao ndio walio wafikishia watu ujumbe wa Mwenyezi Mungu kama tulivyo wateremshia. Nao wanamkhofu Yeye, wala hawamkhofu yeyote asiye kuwa Yeye. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Yeye ndiye Muangalizi Mwenye kuhisabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha Allah Mtukufu, Aliyetakasika, Aliwataja Manabii waliopita na Akawasifu kwamba wao ni wale wanaozifikisha jumbe za Allah Mtukufu kwa watu, na wanamuogopa Allah Mtukufu, Peke Yake, na hawamuogopi yoyote asiyekuwa Yeye. Na inatosha kuwa Allah Mtukufu ni mwenye kuwahesabu waja Wake kwa matendo yao yote na ni Mwenye kuyaona.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net