Al-Ahzaab 33:36
الأحزابوَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥٓ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ ٱلْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَـٰلًا مُّبِينًا
Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na hiari katika jambo lao, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri katika jambo. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika amepotea upotovu ulio wazi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi. [36]
[36] Haimjuzii Muumini, mwanamume au mwanamke, kuwa na khiari katika jambo lolote baada ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake wakisha lihukumia. Na mwenye kwenda kinyume na alivyo hukumu Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi amejitenga mbali na njia iliyo sawa kwa umbali ulio dhaahiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na haipasi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke iwapo Allah Mtukufu na Mtume Wake wametoa uamuzi wawe wataenda kinyume nao, kwa kuchagua lile ambalo silo alilolihukumu kwao. Na anayemuasi Allah Mtukufu na Mtume Wake, amekuwa mbali na njia ya sawa umbali ulio wazi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net