Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 35

Al-Ahzaab 33:35

الأحزاب

إِنَّ ٱلْمُسْلِمِينَ وَٱلْمُسْلِمَـٰتِ وَٱلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَـٰتِ وَٱلْقَـٰنِتِينَ وَٱلْقَـٰنِتَـٰتِ وَٱلصَّـٰدِقِينَ وَٱلصَّـٰدِقَـٰتِ وَٱلصَّـٰبِرِينَ وَٱلصَّـٰبِرَٰتِ وَٱلْخَـٰشِعِينَ وَٱلْخَـٰشِعَـٰتِ وَٱلْمُتَصَدِّقِينَ وَٱلْمُتَصَدِّقَـٰتِ وَٱلصَّـٰٓئِمِينَ وَٱلصَّـٰٓئِمَـٰتِ وَٱلْحَـٰفِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَٱلْحَـٰفِظَـٰتِ وَٱلذَّٰكِرِينَ ٱللَّهَ كَثِيرًا وَٱلذَّٰكِرَٰتِ أَعَدَّ ٱللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا

Maana

Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na wanaume watiifu na wanawake watiifu, na wanaume wakweli na wanawake wakweli, na wanaume wanaosubiri, na wanawake wanaosubiri, na wanaume wanyenyekevu na wanawake wanyenyekevu, na wanaume watoao sadaka na wanawake watoao sadaka, na wanaume wanaofunga saumu na wanawake wanaofunga saumu, na wanaume wanaojihifadhi tupu zao, na wanawake wanaojihifadhi tupu zao, na wanaume wanaomdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi na wanawake wanaomdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi, Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na ujira mkubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na wat'iifu wanaume na wat'iifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wanawake, na wanao subiri wanaume na wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanawake, na watoao sadaka wanaume na wanawake, na wanao funga wanaume na wanawake, na wanao jihifadhi tupu zao wanaume na wanawake, na wanao mdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi wanaume na wanawake, Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na ujira mkubwa. [35]

[35] Hakika wenye kut'ii miongoni mwa wanaume na wanawake, na wenye kumsadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wanaume na wanawake, na wenye kusimama kwa ut'iifu wanaume na wanawake, na walio wa kweli katika kauli zao na vitendo vyao katika wanaume na wanawake, na wenye kusubiri katika kubeba mashaka kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wanaume na wanawake, na wanyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu wanaume na wanawake, na wenye kuzihifadhi tupu zao kwa yasiyo kuwa halali wanaume na wanawake, na wenye kumdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi katika nyoyo zao na ndimi zao wanaume na wanawake, Mwenyezi Mungu amewaandalia kuwasamehe madhambi yao, na kuwalipa malipo makubwa kwa vitendo vyao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale wanaume na wanawake wenye kufuata amri za Allah Mtukufu, na wanaume na wanawake wenye kuamini, na wanaume na wanawake wenye kumtii Allah Mtukufu na Mtume Wake, na wakweli wa kiume na wa kike, na wanaume na wanawake wenye kusubiri katika kujiepusha na matamanio na juu ya kufanya matendo ya utiifu na juu ya shida, na wanaume na wanawake wenye kumcha Allah Mtukufu, na wanaume na wanawake wenye kutoa sadaka za lazima na za ziada, na wanaume na wanawake wenye kufunga saumu za lazima na za ziada, na wanaume na wanawake wenye kuzihifadhi tupu zao na uzinifu na vitangulizi vyake na kujihifadhi ufunuaji uchi, na wanaume na wanawake wenye kumtaja Allah Mtukufu kwa wingi kwa nyoyo zao na ndimi zao, Hao Allah Mtukufu Amewaandalia msamaha wa dhambi zao na malipo mema makubwa, nayo ni Pepo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net