Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 34

Al-Ahzaab 33:34

الأحزاب

وَٱذْكُرْنَ مَا يُتْلَىٰ فِى بُيُوتِكُنَّ مِنْ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ وَٱلْحِكْمَةِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ لَطِيفًا خَبِيرًا

Maana

Na kumbukeni yasomwayo majumbani mwenu katika Aya za Mwenyezi Mungu na hekima. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo ya siri, na Mwenye habari.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kumbukeni yasomwayo majumbani mwenu katika Aya za Mwenyezi Mungu na hikima. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo ya siri, na Mwenye khabari. [34]

[34] Na hifadhini yanayo somwa katika nyumba zenu ya Qur'ani aliyo iteremsha Mwenyezi Mungu, na hikima zilio sawa za Mtume wa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua mambo yalio zama ndani kabisa na ya hakika yake. Basi tahadharini na kwenda kinyume naye na kumuasi Mtume wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na yatajeni yale yanayosomwa ndani ya majumba yenu, ya Qur’ani na hadithi za Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie) na muyafanyie kazi na myape cheo ambacho yanastahiki, kwani hayo ni miongoni mwa neema za Allah Mtukufu kwenu. Hakika Allah Mtukufu ni Mpole kwenu, kwa kuwa Amewaweka kwenye nyumba ambazo aya za Allah Mtukufu zinasomwa na Sunnah, ni Mtambuzi wa kuwatambua nyinyi kwa kuwachagua muwe wake wa Mtume Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net