Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 31

Al-Ahzaab 33:31

الأحزاب

وَمَن يَقْنُتْ مِنكُنَّ لِلَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَتَعْمَلْ صَـٰلِحًا نُّؤْتِهَآ أَجْرَهَا مَرَّتَيْنِ وَأَعْتَدْنَا لَهَا رِزْقًا كَرِيمًا

Maana

Na miongoni mwenu atakayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akatenda mema, tutampa malipo yake mara mbili, na tutamwandalia riziki ya ukarimu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

NA MIONGONI mwenu atakeye mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akatenda mema, tutampa malipo yake mara mbili, na tutamwandalia riziki ya ukarimu. [31]

[31] Na katika nyinyi mwenye kudumu juu ya kumnyenyekea Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akatenda mema, Mwenyezi Mungu atampa ujira mara mbili. Na tumemuandalia kwa Akhera riziki ya kipimo kizuri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mwenye kumtii Allah Mtukufu na Mtume Wake kati yenu na akafanya matendo Aliyoyaamrisha Allah Mtukufu, tutampa malipo mema ya matendo yake mara mbili zaidi ya malipo ya asiyekuwa yeye kati ya wanawake wengine, na tumemuandalia yeye riziki nzuri, nayo ni Pepo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net