Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 32

Al-Ahzaab 33:32

الأحزاب

يَـٰنِسَآءَ ٱلنَّبِىِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِّنَ ٱلنِّسَآءِ ۚ إِنِ ٱتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِٱلْقَوْلِ فَيَطْمَعَ ٱلَّذِى فِى قَلْبِهِۦ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا

Maana

Enyi wake wa Nabii, nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine. Kama mnamcha Mungu, basi msilegeze sauti zenu, akaingia tamaa mwenye maradhi katika moyo wake. Na semeni maneno mema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine. Kama mnamcha Mungu basi msiregeze sauti zenu, akaingia tamaa mwenye maradhi katika moyo wake. Na semeni maneno mema. [32]

[32] Enyi wake wa Mtume! Nyinyi si kama wanawake wengine kwa fadhila na utukufu. Kama mnataka uchamngu, basi msizungumze kwa maneno ya kuregeza sauti, hata ambaye ana uharibifu katika moyo wake akaingia tamaa. Kusema kwenu kuwe kama kawaida sio kujitia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi wake wa Nabii! Nyinyi, katika utukufu na cheo, si kama wanawake wasiokuwa nyinyi iwapo mtafanya matendo ya utiifu kwa Allah Mtukufu na Mtume Wake na mtajiepusha na mambo ya kumuasi yeye. Basi msizungumze na wanaume wa kando kwa sauti nyororo yenye kumtia tamaa mwanamume ambaye kuna ubaya ndani ya moyo wake na ugonjwa wa kutamani haramu, (Hii ni adabu ya lazima kwa kila mwanamke Anayemuamini Allah Mtukufu na Siku ya Mwisho.) na semeni maneno yaliyo mbali na shaka yasiyokatazwa na Sheria.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net