Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 30

Al-Ahzaab 33:30

الأحزاب

يَـٰنِسَآءَ ٱلنَّبِىِّ مَن يَأْتِ مِنكُنَّ بِفَـٰحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ يُضَـٰعَفْ لَهَا ٱلْعَذَابُ ضِعْفَيْنِ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرًا

Maana

Enyi wake wa Nabii, atakayefanya uchafu dhahiri miongoni mwenu, atazidishiwa adhabu mara mbili. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi wake wa Nabii! Atakaye fanya uchafu dhaahiri miongoni mwenu, atazidishiwa adhabu mara mbili. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi. [30]

[30] Enyi wake wa Nabii! Miongoni mwenu mwenye kufanya makosa yaliyo dhaahiri ubaya wake, basi juu ya adhabu yake zinaongezwa adhabu mbili, ili iwe adhabu tatu kwa kulinganisha na mwenziwe. Na kuongeza huko kwa Mwenyezi Mungu ni kwepesi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi wake za Mtume! Yoyote miongoni mwenu Atakayefanya maasia yaliyo wazi ataongezewa adhabu mara mbili zaidi. Na kwa kuwa cheo chao ni cha juu, imenasibiana na cheo hicho Allah Mtukufu Alifanye dhambi linalotokana na wao liwe zito, ili kuhifadhi heshima yao na heshima ya Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), Na kuadhibu huko ni rahisi kwa Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net