Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 29

Al-Ahzaab 33:29

الأحزاب

وَإِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَٱلدَّارَ ٱلْـَٔاخِرَةَ فَإِنَّ ٱللَّهَ أَعَدَّ لِلْمُحْسِنَـٰتِ مِنكُنَّ أَجْرًا عَظِيمًا

Maana

Na ikiwa mnamtaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya Akhera, basi Mwenyezi Mungu amewaandalia wafanyao mema, miongoni mwenu, malipo makubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ikiwa mnamtaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya Akhera, basi Mwenyezi Mungu amewaandalia wafanyao mema, miongoni mwenu, malipo makubwa. [29]

[29] Na ikiwa mnakhiari mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na neema za nyumba ya Akhera, na mnaridhi maisha magumu mlio nayo hivi sasa, basi hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia mfano wenu nyinyi miongoni mwa wanawake walio wema kwa vitendo vyao, ujira ambao haukadiriki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mkiwa mnataka radhi za Allah Mtukufu na Mtume Wake na yale aliyowaandalia Allah Mtukufu katika Nyumba ya Akhera, basi vumilieni juu ya hali mliyonayo, na mtiini Allah Mtukufu na Mtume Wake, kwani hakika Allah Mtukufu Amewaandalia walio wema katika nyinyi malipo makubwa. (Na walimchagua Allah Mtukufu na Mtume Wake na yale Aliyowaandalia Allah Mtukufu katika Nyumba ya Akhera).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net