Al-Ahzaab 33:28
الأحزابيَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ قُل لِّأَزْوَٰجِكَ إِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَيْنَ أُمَتِّعْكُنَّ وَأُسَرِّحْكُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا
Ewe Nabii! Waambie wake zako: Ikiwa mnataka maisha ya dunia na pambo lake, basi njooni, nitawapa kutoka nyumba, na kuwaacha mwachano mzuri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ewe Nabii! Waambie wake zako: Ikiwa mnataka maisha ya dunia na pambo lake, basi njooni, nitakupeni kitoka nyumba, na kukuacheni mwachano mzuri. [28]
[28] Ewe Nabii! Waambie wake zako kwa kuwanasihi: Ikiwa mnataka maisha ya duniani na starehe zake, basi jongeeni nitakupeni cha kupunguza upweke wa talaka, itakuwa ni tunza yenu. Na nitakupeni talaka isiyo na uovu ndani yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ewe Nabii! Waambie wake zako waliojikusanya mbele yako wakitaka kwako ongezo la matumizi, «Mkiwa mnataka maisha ya kilimwengu na pambo lake, basi njooni niwastareheshe kwa kitu kichache cha kilimwengu nilicho nacho na niwatenge bila ya kuwadhuru wala kuwaudhi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net