Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 27

Al-Ahzaab 33:27

الأحزاب

وَأَوْرَثَكُمْ أَرْضَهُمْ وَدِيَـٰرَهُمْ وَأَمْوَٰلَهُمْ وَأَرْضًا لَّمْ تَطَـُٔوهَا ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرًا

Maana

Na akawarithisha ardhi zao na nyumba zao na mali zao, na ardhi msiyopata kuikanyaga. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na akakurithisheni ardhi zao na nyumba zao na mali zao, na ardhi msiyo pata kuikanyaga. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. [27]

[27] Na akakurithisheni ardhi zao, na nyumba zao, na mali zao, na ardhi ambazo nyayo zenu hazijapata kuzikanyaga kabla yake. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Muweza wa kutimiza kila alitakalo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Akawamilikisha nyinyi, enyi Waumini, ardhi yao, makazi yao na mali yao yanayohamishika kama vile pambo, silaha na wanyama na yasiyohamishika kama vile mashamba, nyumba na ngome zilizojikita. Na Akawarithisha ardhi ambayo hamkuweza kuikanyaga kabla ya hapo. Na Allah Mtukufu ni Muweza wa kila kitu, hakuna kinachomshinda.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net