Al-Ahzaab 33:26
الأحزابوَأَنزَلَ ٱلَّذِينَ ظَـٰهَرُوهُم مِّنْ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ مِن صَيَاصِيهِمْ وَقَذَفَ فِى قُلُوبِهِمُ ٱلرُّعْبَ فَرِيقًا تَقْتُلُونَ وَتَأْسِرُونَ فَرِيقًا
Na akawateremsha wale waliowasaidia maadui katika Watu wa Kitabu kutoka katika ngome zao, na akatia hofu katika nyoyo zao. Baadhi yao mkawa mnawaua, na wengine mnawateka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na akawateremsha wale walio wasaidia (maadui) katika Watu wa Kitabu kutoka katika ngome zao; na akatia khofu katika nyoyo zao. Baadhi yao mkawa mnawauwa, na wengine mnawateka. [26]
[26] Na Mwenyezi Mungu aliwateremsha walio wasaidia makundi ya maadui katika Watu wa Kitabu, nao ni Mayahudi wa Bani Quraidha, kutokana na ngome zao walipo kuwa wakijilinda ndani yake. Na akaingiza katika nyoyo zao kitisho. Wengine mkawa mnawawauwa, nao ni wanaume, na wengine mnawachukua mateka, nao ni wanawake na watoto.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu Akawateremsha Mayahudi wa Banū Qurayẓah kutoka kwenye ngome zao kwa kuwa waliyasaidia Mapote katika kupigana na Waislamu, na Akatia hofu ndani ya nyoyo zao wakashindwa, mkawa mnaua kundi katika wao na mnateka kundi lingine.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net