Al-Ahzaab 33:25
الأحزابوَرَدَّ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِغَيْظِهِمْ لَمْ يَنَالُوا۟ خَيْرًا ۚ وَكَفَى ٱللَّهُ ٱلْمُؤْمِنِينَ ٱلْقِتَالَ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ قَوِيًّا عَزِيزًا
Na Mwenyezi Mungu aliwarudisha nyuma makafiri juu ya ghadhabu yao; hawakupata heri yoyote. Na Mwenyezi Mungu amewatosheleza Waumini katika vita. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na uweza.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu aliwarudisha nyuma makafiri juu ya ghadhabu yao; hawakupata kheri yoyote. Na Mwenyezi Mungu amewatosheleza Waumini katika vita. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na uweza. [25]
[25] Mwenyezi Mungu akawarudisha nyuma makafiri walio jiunga makundi kumpiga Mtume na nyoyo zao zimejaa chuki. Hawakupata kheri yoyote kwa ushindi wala ngawira. Na Mwenyezi Mungu amewatosheleza Waumini wasipate mashaka, kwa kuwapatiliza wale makafiri kwa upepo na Malaika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza wa kutimiliza alitakalo, ni Mwenye nguvu hapana wa kumshinda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Akayarudisha Allah Mtukufu mapote ya ukafiri kutoka Madina yakiwa yamepita patupu, yamepata hasara na yamejawa na hasira, hayakupata kheri yoyote duniani wala Akhera, na Allah Mtukufu Akawatosheleza Waumini (wasilazimike) kupigana kwa kuwasaidia kwa sababu Alizowatolea. Na Allah Mtukufu ni Mwenye nguvu, Hashindwi wala Halazimishwi, ni Mshindi katika ufalme Wake na mamlaka Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net