Al-Ahzaab 33:24
الأحزابلِّيَجْزِىَ ٱللَّهُ ٱلصَّـٰدِقِينَ بِصِدْقِهِمْ وَيُعَذِّبَ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ إِن شَآءَ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا
Ili Mwenyezi Mungu awalipe wakweli kwa sababu ya ukweli wao, na awaadhibu wanafiki pindi akitaka, au apokee toba yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ili Mwenyezi Mungu awalipe wakweli kwa sababu ya ukweli wao, na awaadhibu wanaafiki pindi akitaka, au apokee toba yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [24]
[24] Ili Mwenyezi Mungu apate kuwalipa Waumini walio wakweli kwa sababu ya ukweli wao katika Imani yao na kutimiza kwao ahadi waliyo itoa. Na awaadhibu wanaafiki - pindi akitaka - au amwezeshe aliye elekea, kufikia toba. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe kwa kukubali toba, Mwenye kurehemu kwa kusamehe maasi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ili Allah Mtukufu Awalipe mema watu wa ukweli kwa ukweli wao na kujitolea kwao, nao ni Waumini, na ili Awaadhibu wanafiki Akitaka kuwaadhibu, kwa kutowapa taufiki ya kutubia toba ya kidhati kabla ya kufa, hivyo basi wafe kwenye ukafiri na wastahili Moto, au Awape taufiki ya kutubia na kurejea, kwani Allah Mtukufu ni Mwingi wa kusamehe dhambi za wenye kuzidhulumu nafsi zao, ni Mwingi wa huruma kwao kwa kuwapa taufiki ya kutubia toba ya kidhati.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net