Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 31 · Aya ya 5

Luqman 31:5

لقمان

أُو۟لَـٰٓئِكَ عَلَىٰ هُدًى مِّن رَّبِّهِمْ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ

Maana

Hao ndio walio kwenye uongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio waliofaulu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao ndio walio na uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio wenye kufanikiwa. [5]

[5] Hao Waumini wanao tenda vyema vitendo vyao, wametua kwenye Uwongofu ulio wajia kutokana na Mola wao Mlezi. Na hao tu - si wengineo - ndio wenye kufuzu kikweli.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hao wanaosifika kwa sifa zilizotangulia wako kwenye ubainifu na nuru kutoka kwa Mola wao, na wao ndio wenye kufaulu ulimwenguni na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Luqman

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net