Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 31 · Aya ya 4

Luqman 31:4

لقمان

ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤْتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَهُم بِٱلْـَٔاخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ

Maana

Wale wanaoshika Swala, na wanatoa Zaka, nao wana yakini na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wanao shika Swala, na wanatoa Zaka, nao wana yakini na Akhera. [4]

[4] Hao ndio wanao timiza Swala kwa njia ya ukamilifu kabisa, na wanawapa Zaka wanao istahiki; na wao wanayaamini maisha ya Akhera kwa imani yenye nguvu kabisa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wanaotekeleza Swala kikamilifu kwa nyakati zake na wanaotoa Zaka zilizo lazima juu yao kwa wanaostahiki kupewa. Na hali wao wana yakini kuwa kuna kufufuliwa na kulipwa Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Luqman

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net