Luqman 31:6
لقمانوَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَشْتَرِى لَهْوَ ٱلْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ
Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu mbali na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni masihara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na miongoni mwa watu wapo wanao nunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha. [6]
[6] Na miongoni mwa watu wapo ambao hununua maneno ya uwongo wawasimulie watu wapate kuwatenga na Uislamu na Qur'ani kwa kutojua dhambi zilio juu yao, na wanaifanyia maskhara Dini ya Mwenyezi Mungu na Ufunuo wake. Watendayo hayo watapata adhabu ya kuwatia unyonge na kuwadhalilisha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na miongoni mwa watu kuna wanaonunua maneno ya pumbao, nayo ni kila chenye kumpumbaza mtu na utiifu wa Allah Mtukufu, ili wawapoteze watu na njia ya uongofu wafuate njia ya matamanio na wazifanye aya za Allah Mtukufu kuwa ni shere, basi hao watakuwa na adhabu yenye kuwadhalilisha na kuwatweza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net