Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 30 · Aya ya 8

Ar-Room 30:8

الروم

أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا۟ فِىٓ أَنفُسِهِم ۗ مَّا خَلَقَ ٱللَّهُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَآ إِلَّا بِٱلْحَقِّ وَأَجَلٍ مُّسَمًّى ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ ٱلنَّاسِ بِلِقَآئِ رَبِّهِمْ لَكَـٰفِرُونَ

Maana

Je, hawajifikirii nafsi zao? Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na vilivyo kati yake isipokuwa kwa Haki na kwa muda maalumu. Na hakika watu wengi bila ya shaka ni wenye kukufuru kuwa watakutana na Mola wao Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Hawajifikirii nafsi zao? Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yake ila kwa Haki na kwa muda maalumu. Na hakika watu wengi bila ya shaka ni wenye kukataa kuwa watakutana na Mola wao Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hawakufikiri, hawa wakanushaji Mitume wa Allah Mtukufu na kukutana na Yeye, vile Allah Mtukufu Alivyowaumba, na kuwa wao Amewaumba na hawakuwa kitu chochote? Allah Mtukufu hakuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake isipokuwa ni kwa ajili ya kusimamisha uadilifu, malipo mema na mateso na kutolea ushahidi upweke Wake na uwezo Wake. Na kwa muda uliotajwa wa kukomea kwake nao ni Siku ya Kiyama. Na kwa hakika, wengi wa watu ni wenye kukataa na kukanusha kwa ujinga wao wa kutojua kuwa marejeo yao ni kwa Allah Mtukufu baada ya kutoweka kwao na kwa kughafilika kwao na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Room

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net