Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 30 · Aya ya 9

Ar-Room 30:9

الروم

أَوَلَمْ يَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَيَنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَانُوٓا۟ أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَأَثَارُوا۟ ٱلْأَرْضَ وَعَمَرُوهَآ أَكْثَرَ مِمَّا عَمَرُوهَا وَجَآءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ ۖ فَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ

Maana

Je, hawatembei katika ardhi wakaona ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Nao walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao, na wakaitimbua ardhi na wakaistawisha zaidi kuliko walivyoistawisha wao. Na Mitume wao wakawajia na ushahidi wa wazi. Basi hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwadhulumu, lakini wenyewe walikuwa wakijidhulumu nafsi zao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Hawatembei katika ardhi wakaona ulivyo kuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Nao walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao, na wakaitimbua ardhi na wakaistawisha zaidi kuliko walivyo istawisha wao. Na Mitume wao wakawajia na dalili zilizo wazi. Basi hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi si waende hawa wanaomkanusha Allah Mtukufu, wanaoghafilika na Akhera, mwendo wa kufikiria na kuzingatia, wakapata kuona yalikuwa namna gani malipo ya ummah waliowakanusha Mitume wa Mwenyezi Mungu, kama vile kina ‘Ãd na Thamûd? Hakika walikuwa wana nguvu zaidi kuliko wao kimiili na wana uwezo zaidi wa kustarehe na maisha, kwa kuwa waliilima ardhi na kuipanda mimea, na wakajenga majumba ya fahari na wakayakalia, hivyo basi waliuimarisha ulimwengu wao kuliko vile watu wa Makkah walivyouimarisha ulimwengu wao, na kusiwafalie kitu kule kuimarisha kwao wala urefu wa maisha yao. Na Mitume wao waliwajia na hoja za wazi na dalili zenye kung’ara, wakawakanusha, na Allah Mtukufu Akawaangamiza. Na Hakuwadhulumu kwa huko kuwaangamiza, isipokuwa wao wenyewe walijidhulumu wenyewe kwa kufanya ushirikina na kuasi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Room

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net