Ar-Room 30:42
الرومقُلْ سِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَٱنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلُ ۚ كَانَ أَكْثَرُهُم مُّشْرِكِينَ
Sema: Safirini duniani na muangalie ulikuwaje mwisho wa wale waliotangulia. Wengi wao walikuwa washirikina.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Safirini duniani muangalie ulikuwaje mwisho wa walio tangulia. Wengi wao walikuwa washirikina.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia wenye kuyakanusha uliyokuja nayo, Tembeeni kwenye sehemu za ardhi matembezi ya kuzingatia na kutia mambo akilini, na mtazame vile ulivyokuwa mwisho wa ummah waliopita wenye kukanusha, kama vile watu wa Nûḥ, ‘Ãd na Thamûd, mtakuta kwamba mwisho wao walioishia ulikuwa mbaya zaidi na kikomo hicho walichokomea kilikuwa kibaya zaidi, kwani wengi wao walikuwa ni wenye kumshirikisha Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net