Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 30 · Aya ya 41

Ar-Room 30:41

الروم

ظَهَرَ ٱلْفَسَادُ فِى ٱلْبَرِّ وَٱلْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِى ٱلنَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ ٱلَّذِى عَمِلُوا۟ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

Maana

Uharibifu umedhihiri barani na baharini kwa yale iliyoyafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonjeshe baadhi ya yale waliyoyatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Uharibifu umejitokeza barani na baharini, kama vile ukame, uchache wa mvua, wingi wa magonjwa na majanga, kwa sababu ya maasia yanayofanywa na binadamu, hivyo basi Awapatie adhabu kwa baadhi ya matendo waliyoyatenda ulimwenguni wapate kutubia kwa Allah Mtukufu, (kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake), na warudi nyuma waache maasia na matendo yao yatengenezeke na mambo yao yalingane sawa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Room

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net