Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 30 · Aya ya 40

Ar-Room 30:40

الروم

ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَكُمْ ثُمَّ رَزَقَكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ۖ هَلْ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَفْعَلُ مِن ذَٰلِكُم مِّن شَىْءٍ ۚ سُبْحَـٰنَهُۥ وَتَعَـٰلَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

Maana

Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaumba, kisha akawaruzuku, kisha atawafisha, na kisha atawafufua. Je, yupo yeyote katika hao mnaowashirikisha na Mwenyezi Mungu afanyae lolote katika hayo? Yeye ametakasika, na ametukuka mbali na hayo mnayomshirikisha naye.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni, kisha akakuruzukuni, kisha anakufisheni, na kisha anakufufueni. Je! Yupo yeyote katika hao mnao washirikisha na Mwenyezi Mungu afanyae lolote katika hayo? Yeye ametakasika, na ametukuka na hayo mnayo mshirikisha naye. [40]

[40] Mwenyezi Mungu Subhaanu Alietakasaika, ndie aliekuumbeni, kisha kakupeni cha kukupeeni maisha, kisha ndie anaekufesheni, na kisha atakufufueni kutoka makaburini mwenu. Je? Yupo yoyote katika hao miungu ya kishirikina mnao dai na mukaawabudu badala ya Mwenyezi Mungu mwenye kutenda hayo ya kuumba na kukuruzuku, na kufisha na kukufua, au kitendo chochote, Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo wanao mshirikisha naye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu, Peke Yake, Ndiye Aliyewaumba nyinyi, enyi watu, kisha Akawapa riziki katika uhai huu, kisha Atawafisha muda wenu ufikapo, kisha Atawafufua kutoka makaburini mkiwa mko hai mpate kuhesabiwa na kulipwa. Je kuna yoyote miongoni mwa washirika wenu anayefanya chochote katika hayo? Ametakasika Allah Mtukufu na ushirikina wa hawa wenye kumshirikisha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Room

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net