Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 30 · Aya ya 39

Ar-Room 30:39

الروم

وَمَآ ءَاتَيْتُم مِّن رِّبًا لِّيَرْبُوَا۟ فِىٓ أَمْوَٰلِ ٱلنَّاسِ فَلَا يَرْبُوا۟ عِندَ ٱللَّهِ ۖ وَمَآ ءَاتَيْتُم مِّن زَكَوٰةٍ تُرِيدُونَ وَجْهَ ٱللَّهِ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُضْعِفُونَ

Maana

Na mnachokitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini mnachokitoa kwa Zaka kwa kutaka uso wa Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watakaozidishiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mnacho kitoa kwa Riba ili kiongozeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini mnacho kitoa kwa Zaka kwa kutaka radhi ta Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watakao zidishiwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mkopo wowote wa pesa mnaoutoa kwa makusudio ya riba, na kutaka kuzidisha mkopo huo ili kupatikane ongezeko katika mali ya watu, basi mbele ya Allah Mtukufu hayaongezeki, bali Anayaondolea baraka na kuyabatilisha. Na Zaka na sadaka mnazotoa kuwapatia wastahiki kwa kutafuta radhi za Allah Mtukufu na kutaka malipo yake, basi hiki ndicho ambacho Allah Mtukufu Anakikubali na Atawaongezea mara nyingi zaidi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Room

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net