Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 30 · Aya ya 38

Ar-Room 30:38

الروم

فَـَٔاتِ ذَا ٱلْقُرْبَىٰ حَقَّهُۥ وَٱلْمِسْكِينَ وَٱبْنَ ٱلسَّبِيلِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يُرِيدُونَ وَجْهَ ٱللَّهِ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ

Maana

Basi mpe jamaa haki yake, na masikini, na msafiri. Hayo ni heri kwa wanaotaka uso wa Mwenyezi Mungu. Na hao ndio waliofaulu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi mpe jamaa haki yake, na masikini, na msafiri. Hayo ni kheri kwa watakao radhi ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio wenye kufanikiwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi mpe, ewe mwenye kuamini, jamaa yako wa karibu haki yake ya kuunga udugu na sadaka na mambo mengine ya wema. Na mpe masikini na mwenye uhitaji aliyekatikiwa na njia (kwa kuishiwa na pesa akiwa safarini) Zaka na sadaka. Kwani kutoa huko ni bora kwa wale wanaoukusudia kupata radhi za Allah Mtukufu kwa matendo yao mema. Na wanaofanya matendo haya na megineyo miongoni mwa matendo mema, wao ndio wenye kufaulu kupata malipo ya Allah Mtukufu, ndio wenye kuokoka na mateso Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Room

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net