Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 30 · Aya ya 37

Ar-Room 30:37

الروم

أَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّ ٱللَّهَ يَبْسُطُ ٱلرِّزْقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ

Maana

Kwani hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na humkunjia amtakaye? Hakika katika hayo, zipo Ishara kwa watu wanaoamini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwani hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na humdhikisha amtakaye? Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanao amini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hawajui kwamba Allah Mtukufu Anamkunjulia riziki Anayemtaka kwa kumjaribu: atashukuru au atakufuru? Na (kwani hawajui kwamba Yeye) Anambania riziki Anayemtaka kwa kumjaribu: je atavumilia au atababaika? Hakika katika kukunjulia na kubania kuna alama (za utendakazi wa Allah Mtukufu) kwa watu wanaomuamini Allah Mtukufu na wanaojua hekima ya Allah Mtukufu na rehema zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Room

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net