Ar-Room 30:43
الرومفَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ ٱلْقَيِّمِ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِىَ يَوْمٌ لَّا مَرَدَّ لَهُۥ مِنَ ٱللَّهِ ۖ يَوْمَئِذٍ يَصَّدَّعُونَ
Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini iliyonyooka kabla ya kufika Siku hiyo isiyozuilika, inayotoka kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo watu watatengana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi uelekeze uso wako kwenye Dini Iliyo Nyooka kabla ya kufika Siku hiyo isiyo zuilika, inayo toka kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo watu watatengana.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi elekeza uso wako, ewe Mtume, upande wa Dini iliyonyooka, nayo ni Uislamu, hali ya kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha makatazo yake. Na ushikamane nayo kabla Siku ya Kiyama haijaja, kwani ijapo Siku hiyo, ambayo hakuna anayeweza kuirudisha, viumbe watapambanuka wakiwa makundi makundi yalio tafauti ili waoneshwe matendo yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net