Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 6

Aal-i-Imraan 3:6

آل عمران

هُوَ ٱلَّذِى يُصَوِّرُكُمْ فِى ٱلْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَآءُ ۚ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ

Maana

Yeye ndiye anayewaunda ndani ya matumbo ya uzazi kwa namna apendavyo. Hakuna mungu isipokuwa Yeye, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye ndiye anaye kuundeni ndani ya matumbo ya wazazi kwa namna apendayo. Hapana Mungu ila Yeye, Mwenye nguvu na Mwenye hikima. [6]

[6] Ni Yeye, Mwenyezi Mungu, ndiye anakuundeni, anakupeni sura na hali nyinyi mmo matumboni mwa mama zenu, kwa sura na umbo mbali mbali kama apendavyo Yeye. Hapana Mungu ila Yeye Mwenye nguvu katika ufalme wake, Mwenye hikima katika kuunda kwake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yeye Peke Yake Ndiye Ambaye Anawaumba Nyinyi katika zao za mamama zenu kama Atakavyo: wanaume, wanawake, wazuri, wabaya, waovu na wema. Hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, Mshindi Asiyeshindwa, Mwenye hekima katika amri Zake na uendeshaji mambo Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net