Aal-i-Imraan 3:5
آل عمرانإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَخْفَىٰ عَلَيْهِ شَىْءٌ فِى ٱلْأَرْضِ وَلَا فِى ٱلسَّمَآءِ
Hakika, Mwenyezi Mungu hakifichikani chochote kwake, katika dunia wala katika mbingu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Mwenyezi Mungu hakifichiki chochote kwake, duniani wala mbinguni. [5]
[5] Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. Kwa hivyo hapana kinacho fichika kwake katika Ardhi na hata katika Mbingu, kikiwa kidogo au kikubwa, kinacho onekana na kisicho onekana.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Allah Mtukufu, ujuzi Wake umewazunguka viumbe wote. Hakuna kitu chenye kufichika Kwake katika ardhi wala katika mbingu, kiwe kichache au kingi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net