Aal-i-Imraan 3:4
آل عمرانمِن قَبْلُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ ٱلْفُرْقَانَ ۗ إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ ذُو ٱنتِقَامٍ
Kabla yake, viwe uongofu kwa watu. Na akateremsha Furqani (Upambanuo). Hakika, wale waliozikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu wana adhabu kali. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kulipiza.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kabla yake, ziwe uwongofu kwa watu. Na akateremsha Furqani (Upambanuo). Hakika walio zikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu watakuwa na adhabu kali. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye kulipa. [4]
[4] Ameziteremsha hizo kabla ya Qur'ani ili kuwaongoa watu. Walipo kengeuka akaiteremsha Qur'ani ipambanue baina ya Haki na baat'ili, baina ya kweli na uwongo, baina ya uwongofu na upotovu. Basi hii Qur'ani ni Kitabu cha kweli, chenye kudumu milele. Na kila mwenye kuacha aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu na akazikanya Aya zake, Ishara zake, atapata adhabu iliyo kali. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza, hashindwi na kitu, na Mwenye kuwalipa wanao stahiki kulipwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
kabla ya kuteremka Qur’ani, ili kuwaongoza Wacha Mungu kwenye Imani na kutengeneza dini yao na dunia yao. Na Aliteremsha yenye kupambanua baina ya haki na batili. Na wale ambao wamekanusha aya za Allah Mtukufu zilizoteremshwa, wana adhabu kubwa. Na Allah Mtukufu ni Mshindi Asiyeshindwa, ni Mwenye kumtesa anayezikanusha hoja na dalili Zake na kupwekeka Kwake kwa uungu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net