Aal-i-Imraan 3:49
آل عمرانوَرَسُولًا إِلَىٰ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ أَنِّى قَدْ جِئْتُكُم بِـَٔايَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ أَنِّىٓ أَخْلُقُ لَكُم مِّنَ ٱلطِّينِ كَهَيْـَٔةِ ٱلطَّيْرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيْرًۢا بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۖ وَأُبْرِئُ ٱلْأَكْمَهَ وَٱلْأَبْرَصَ وَأُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰ بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۖ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِى بُيُوتِكُمْ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ
Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Mimi kwa hakika nimewajia na Ishara kutoka kwa Mola wenu Mlezi, ya kwamba mimi kwa hakika ninawaundia kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha ninapuliza ndani yake na anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaambia mnachokila na mnachoweka akiba katika nyumba zenu. Hakika, katika haya ipo Ishara kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Mimi nimekujieni na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu, ya kwamba nakuundieni kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho weka akiba katika nyumba zenu. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwi nyinyi ni wenye kuamini. [49]
[49] Na atamtuma awe Mtume wake kwa Wana wa Israili, (Katika Injili ya Mathayo 15.24 Yesu anasema: Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.- Tazama pia Mathayo 10.5-6 na Mathayo 19.28 na Yohana 17.9) mwenye kutumia hoja za ukweli wa Utume wake kwa miujiza kutokana na Mwenyezi Mungu. Miujiza yenyewe ni kama kufanya kwa udongo sura ya ndege, kisha akipulizia vitaingia uhai na kutaharaki mithili ya ndege kwa atakavyo Mwenyezi Mungu. Pia ataponyesha, kwa kudra ya Mwenyezi Mungu, walio zaliwa vipofu na wataona, na wenye maradhi ya ukoma waondokewe na ukoma, na walio onekana wamekwisha kufa wafufuke. Na yote hayo ni kwa idhini na matakwa ya Mwenyezi Mungu. Pia atawatajia wanacho weka akiba majumbani mwao, vyakula na vyenginevyo. Naye Nabii Isa awaambie: Ishara zote hizi Mwenyezi Mungu amezionyesha kwangu ili iwe hoja kuwa Utume wangu ni wa haki, ikiwa nyinyi ni katika watu wanao t'ii na kusadiki.(Katika Injili ya Yohana 5.30 Yesu anasema: Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe.)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Atamjaalia awe Mtume kwa Wana wa Isrãîl na atawaambia wao, Mimi nimewajia na alama kutoka kwa Mola wenu inayoonesha kuwa mimi nimetumilizwa kutoka kwa Allah Mtukufu. Nayo ni kuwa nitawafanyia kwa udongo kitu chenye mfano wa ndege, nitapuliza ndani yake na kitakuwa ndege wa kikweli kwa idhini ya Allah Mtukufu. Na nitamponya aliyezaliwa kipofu na mwenye barasi na nitamhuisha aliyekufa kwa idhini ya Allah Mtukufu. Na nitawaambia chakula mnachokula na mnachoweka akiba majumbani mwenu. Hakika katika mambo makubwa haya, ambayo hayako kwenye uwezo wa wanaadamu, pana dalili kwamba mimi ni Nabii wa Allah Mtukufu na Mtume Wake, iwapo nyinyi ni wenye kuamini hoja za Allah Mtukufu na alama Zake, ni wenye kukiri kumpwekesha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net