Aal-i-Imraan 3:50
آل عمرانوَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَىَّ مِنَ ٱلتَّوْرَىٰةِ وَلِأُحِلَّ لَكُم بَعْضَ ٱلَّذِى حُرِّمَ عَلَيْكُمْ ۚ وَجِئْتُكُم بِـَٔايَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Na ninasadikisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na ili niwahalalishie baadhi ya yale mliyoharamishiwa. Na nimewajia na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu. Kwa hivyo, mcheni Mwenyezi Mungu na nitiini mimi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ninasadikisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale mlio harimishiwa, na nimekujieni na Ishara kutokana na Mola Mlezi wenu. Kwa hivyo mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi. [50]
[50] Na mimi nimetumwa kwenu nisadikishe sharia ya Taurati aliyo teremshiwa Musa, na nikuhalalishieni, kwa amri ya Mwenyezi Mungu, baadhi ya mliyo harimishiwa zamani. Na mimi nimekuja na ishara kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuthibitisha ukweli wa ujumbe wangu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi.(Katika Injili ya Mathayo 5.17 Yesu anasema: Msidhani ya kuwa nilikuja kuitangua torati au manabii, la, sikuja kutangua, bali kutimiza.)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na nimewajia nyinyi kuyasadikisha yaliyomo ndani ya Taurati, na ili niawahalalishie, kwa wahyi unaotoka kwa Allah Mtukufu, baadhi ya yale ambayo Allah Mtukufu Aliwaharamishia, yakiwa ni usahilishaji na huruma kutoka kwa Allah Mtukufu, na nimewajia na hoja kutoka kwa Mola wenu ya ukweli wa ninayowaambia. Basi Mcheni Allah Mtukufu na msiende kinyume na amri Yake na mnitii mimi katika yale ninayowafikishia kutoka kwa Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net