Aal-i-Imraan 3:48
آل عمرانوَيُعَلِّمُهُ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحِكْمَةَ وَٱلتَّوْرَىٰةَ وَٱلْإِنجِيلَ
Na atamfundisha kuandika na hekima na Taurati na Injili.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na atamfunza kuandika na Hikima na Taurati na Injili. [48]
[48] Na Mwenyezi Mungu atamfunza mtoto huyu aliye zaliwa kuandika, na ilimu njema yenye manufaa, na Taurati, Kitabu cha Musa a.s., na Injili atayo mfunulia yeye.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Atamfundisha kuandika, njia ya kuufikia usawa katika kusema na kutenda, Taurati ambayo Allah Mtukufu Alimletea Mûsã, amani imshukie, kwa njia ya wahyi, na Injili ambayo Allah Mtukufu Alimteremshia yeye.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net