Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 47

Aal-i-Imraan 3:47

آل عمران

قَالَتْ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِى وَلَدٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِى بَشَرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكِ ٱللَّهُ يَخْلُقُ مَا يَشَآءُ ۚ إِذَا قَضَىٰٓ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

Maana

Maryam akasema: Mola wangu Mlezi! Vipi nitampata mwana ilhali hajanigusa mwanadamu? Akasema: Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu, yeye huumba atakavyo. Anapohukumu jambo, yeye kwa hakika huliambia: 'Kuwa!' Na linakuwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Maryamu akasema: Mola wangu Mlezi! Vipi nitampata mwana na hali hajanigusa mwanaadamu? Mwenyezi Mungu akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Mwenyezi Mungu huumba apendacho. Anapo hukumu jambo, huliambia: Kuwa! Likawa. [47]

[47] Maryamu alisema kwa kustaajabu kupata mwana kwa njia isiyo ya kawaida: Vipi nitapata mwana na ilhali hapana mwanamume aliyenigusa? (yaani aliye lala nami). Mwenyezi Mungu Mtukufu akakumbusha kuwa Yeye huumba atakacho kwa kudra yake bila ya shuruti za sababu zilizo zowewa. Kwani Yeye akitaka jambo hulileta tu kwa taathira ya uwezo wake katika atakalo bila ya kutafuta kinginecho cha kutimiza matakwa yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Maryam alisema kwa kustaajabu, «Vipi mimi nitakuwa na mtoto na sina mume wala si malaya?» Malaika akamuambia, Tukio hili kwako si jambo lililo mbali kwa Allah Mtukufu Muweza Ambaye Anakipatisha chochote anachokitaka kutokana na kisichokuweko. Akitaka kitu chochote kipatikane Anakiambia, «Kuwa,» nacho kinakuwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net