Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 40

Aal-i-Imraan 3:40

آل عمران

قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِى غُلَـٰمٌ وَقَدْ بَلَغَنِىَ ٱلْكِبَرُ وَٱمْرَأَتِى عَاقِرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكَ ٱللَّهُ يَفْعَلُ مَا يَشَآءُ

Maana

Zakariya akasema: Mola wangu Mlezi! Vipi nitapata mwana, ilhali tayari uzee umeshanifikia, na mke wangu ni tasa? Akasema: Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu, yeye hufanya apendavyo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema Zakariya: Mola wangu Mlezi! Vipi nitapata mwana na hali ukongwe umenifikia, na mke wangu ni tasa? Akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo. [40]

[40] Basi Zakariya alipo pewa bishara hii, ya kupata mwana, alimwelekea Mola Mlezi wake kwa shauku ya kutaka kujua vipi yatakuwa hayo, ya kuwa na mwana na ilhali yeye hanazo njia zijuulikanazo, kwa kuwa yeye mwenyewe kesha konga, na mkewe ni tasa. Mwenyezi Mungu akamjibu kuwa Yeye anapo taka jambo ama huzileta njia au huumba bila ya njia zinazo juulikana. Kwani Yeye hutenda apendavyo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Zakariyyã akasema akiwa na furaha na kwa kustaajabu, «Mola wangu! Vipi nitakuwa na mtoto hali ya kuwa uzee umenifikia hadi ya kunifikia na mke wangu ni tasa, hazai»? Akasema, «Hivyo ndivyo Allah Mtukufu Anavyofanya Anayoyataka katika mambo ya ajabu yanayokwenda kinyume na mambo ya kawaida».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net