Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 39

Aal-i-Imraan 3:39

آل عمران

فَنَادَتْهُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ وَهُوَ قَآئِمٌ يُصَلِّى فِى ٱلْمِحْرَابِ أَنَّ ٱللَّهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَىٰ مُصَدِّقًۢا بِكَلِمَةٍ مِّنَ ٱللَّهِ وَسَيِّدًا وَحَصُورًا وَنَبِيًّا مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ

Maana

Kwa hivyo, Malaika wakamwita hali ya kuwa amesimama katika chumba akisali kwamba: Mwenyezi Mungu anakupa bishara njema ya Yahya, atakayesadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni bwana, na mtawa, na ni Nabii miongoni mwa walio wema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Alipo kuwa kasimama chumbani akiswali, Malaika kamnadia: Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya, ataye kuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni bwana na mt'awa na Nabii kwa watu wema. [39]

[39] Mwenyezi Mungu aliitikia dua yake. Malaika akamnadia naye kasimama pahala pake pa ibada akimwelekea Mola wake Mlezi kumbashiria mtoto mwanamume jina lake Yahya, atakaye muamini Isa a.s. ambaye atazaliwa kwa kauli ya Mwenyezi Mungu kwa njia isiyo ya dasturi. Na Yahya atawahimiza kaumu yake kushika ilimu na kuswali, na atakataza mambo ya pumbao na matamanio, na atamfanya awe miongoni mwa Manabii na watu wema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hapo Malaika walimuita, naye yuko katika hali ya kusimama mbele ya Allah Mtukufu katika mahali pake pa Swala, huku anamuomba Yeye, wakamuambia. «Allah Mtukufu Anakupa habari yenye kukufurahisha, nayo ni kwamba utaruzukiwa mtoto ambaye jina lake ni Yaḥyã, ambaye atalisadikisha neno la Allah Mtukufu, naye ni ‛Ĩsã mwana wa Maryam, amani imshukie. Huyo Yaḥyã atakuwa ni bwana wa kaumu yake, atakuwa na cheo na daraja kubwa, atakuwa ni mwenye kujihifadhi: hatendi madhambi wala hafuati matamanio ya kudhuru na atakuwa ni Nabii miongoni mwa watu wema ambao walifikia kilele cha wema».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net