Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 38

Aal-i-Imraan 3:38

آل عمران

هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُۥ ۖ قَالَ رَبِّ هَبْ لِى مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ ٱلدُّعَآءِ

Maana

Pale pale Zakariya akamwomba Mola wake Mlezi, akasema: Mola wangu Mlezi! Nitunuku kutoka kwako dhuria njema. Hakika, Wewe ndiye unayesikia maombi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Pale pale Zakariya akamwomba Mola wake Mlezi, akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unaye sikia maombi. [38]

[38] Zakariya a.s. alipo iona neema ya Mwenyezi Mungu kwa Maryamu alimwelekea Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu akimwomba kwa fadhila yake na ukarimu wake na uwezo wake, naye ampe mtoto mwanamume. Kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia maombi ya mwenye kuomba kwake kwa unyenyekevu. Naye ni Muweza wa kuitikia maombi na hata zinge kuwapo pingamizi za kikawaida kama ukongwe na utasa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Alipoona Zakariyyã vile Allah Mtukufu Alivyomkirimu Maryam kwa riziki Yake na fadhila Zake, alielekea kwa Mola wake akisema, «Ewe Mola wangu, nipe kutoka Kwako mtoto mwema mwenye kubarikiwa. Wewe ni Msikizi wa maombi ya anayekuomba».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net